Home Back

Dk.Nchimbi-viongozi CCM tengenezeni ramani ya kupata viongozi bora

ippmedia.com 2024/7/7
KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk.Emmanue Nchimbi.

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk.Emmanue Nchimbi.

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk.Emmanue Nchimbi, amewataka viongozi wa chama hicho kutengeneza ramani nzuri ya kupata viongozi bora katika uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka huu na uchaguzi mkuu utakaofanyika 2025.

Akizungumza leo (Mei 30, 2024) na viongozi wa CCM na Serikali wa wilaya zote za Mkoa wa Singida, amesema viongozi wasikubari kuyumbushwa na wachague watu ambao watakuwa tayari kuwatumikia wananchi.

"Viongozi mkatae kutumika,wapimeni watu kwa utu wao sio kwa fedha zake na mtambue kuwa uongozi sio sawa na kampuni kwamba unaweza ukaamua jambo lako mwenyewe bila kuwashirikisha wanachama," amesema.

Dk.Nchimbi amesema suala la viongozi kufanya kazi kwa ushirikishwaji sio jambo la hiari na kwamba chama cha siasa sio kampuni ya mtu binafsi na kuchagua na kuchaguliwa ni haki ya kila mwanachama.

People are also reading