Home Back

Yanga Yathibitisha kuachana na kiungo mshambuliaji Augustine Okrah

globalpublishers.co.tz 2024/10/5
Augustine Okrah

Klabu ya Yanga imethibitisha kuachana na kiungo mshambuliaji Augustine Okrah hivyo hatakuwa sehemu ya kikosi chao msimu ujao 2024-2025.

Okrah raia wa Ghana alitua Yanga Januari 2024 akitokea Bechem United ya Ghana na kuitumikia timu kwa kipindi cha miezi sita akifanikiwa kufunga bao moja tu.

Okrah ambaye pia alipitia Simba Sc akisajiliwa kutoka kutoka Bechem United na kudumu kwa msimu mmoja tu kabla ya kuachana na Wekundu hao wa Msimbazi na kurejea Bechem United na baadaye Yanga Sc kuinasa saini yake.

People are also reading