Home Back

Aziz Ki aipa sharti zito Yanga

spotileo.co.tz 2024/10/5

INADAIWA kuwa Klabu ya Yanga imefikia makubaliano ya kumuongeza mkataba wa kusalia klabuni hapo kiungo wao Stephane Aziz Ki ambaye ametoa masharti kwa uongozi wa klabu, kubwa akihitaji kurejeshwa kwa kiungo mwenzake wa kimataifa wa Burkinafaso, Yacouba Sogne.

Ikumbukwe kuwa Aziz Ki alitua nchini kuchukuwa nafasi ya Yacouba ambaye aliandamwa na majeraha na kumpisha mfungaji bora huyo wa msimu uliomalizika ambaye mkataba wake umefikia tamati na inalezwa kuwa tayari amekubali kusaini mkataba mwingine.

Taarifa zilizoifikia Spotileo kuwa nyota huyo amewapa masharti ya kutaka kuongezewa dau la usajili pamoja na mshahara kubwa pamoja na kurejeshwa kwa Yacouba.

“Ni kweli bado Aziz Ki hajaongeza mkataba na Yanga, licha ya kuwepo kwa mazungumzo hayo ya kuendelea kusalia ndani ya timu hiyo, kuna mambo ametaka kufanyiwa ikiwemo kurejea kwa rafiki yake ndani ya kikosi hicho,” kimesema chanzo chetu cha habari.

Amesema tayari injinia Hersi ameridhia baadhi ya masharti ikiwemo suala la kumuongeza fedha za usajili na mshahara huku mazungumzo ya kurejeshwa Yacouba yakiendelea kufanyika.

Chanzo hicho kimesema kama mambo yataenda vizuri Yacouba atarejea ndani ya kikosi cha yanga kwa mkataba wa miaka miwili.

People are also reading