Home Back

Waziri alia siasa kushamiri matukio manane ya utekaji 2024

mwanahalisionline.com 3 days ago

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni amesema katika kipindi cha mwaka huu kuanzia Januari kumetokea matukio manane ya utekaji na asilimia kubwa ya watuhumiwa wa utekaji huo wamekamatwa na kufikishwa mahakamani. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Akizungumza katika uzinduzi wa kitabu cha Sheikh Mkuu wa Tanzania, Mufti Abubakar  Zubeir ameeleza kushangazwa na siasa kuingizwa katika mtukio hayo kwa kuyahusisha na vyombo vya dola ambavyo jukumu lake ni kulinda raia na mali zao.

Amesisitiza kuwa vyombo vya usalama vina uwezo wa kutosha kukamata watuhumiwa wote wa utekaji na kudhibiti matukio hayo.

Hamad Yusuf Masauni, Waziri wa Mambo ya Ndani Tanzania

Masauni ametoa kauli hiyo wakati Tanzania ikizizima kuhusu tukio la utekaji alilofanyiwa kijana Edgar Mwakabela, maarufu kama Sativa anayedaiwa kutekwa, kuteswa na kutupwa katika pori la Hifadhi ya Katavi akiwa na majeraha mbalimbali mwilini.

Sativa ambaye anaendelea na matibabu katika hospitali ya Aga Khan kuanzia usiku wa tarehe 30 Juni mwaka huu, alidaiwa kutoweka tarehe 23 Juni mwaka huu na kupatikana tarehe 27 Juni mwaka huu katika pori hilo.

Hata hivyo, alipopatikana Sativa anadai alitekwa na watu wasiojulikana na kupelekwa kwenye karakana iliyopo Kituo cha Polisi Oysterbay Dar es Salaam kabla ya kusafirishwa kupelekwa Katavi.

Tyari Rais Samia Suluhu Hassan amesema yeye binafsi atabeba gharama zote za matibabu yake pamoja na uchunguzi wa tukio hilo.

Matukio mengine ni pamoja na Mtoto Albino Asimwe Novart aliyeuawa Wilayani Muleba Mkoani Kagera Mei mwaka huu kabla ya mwili wakekupatikana Juni.

Hata hivyo, watuhumiwa tisa akiwamo baba yake tayari wamekamatwa wakiwa na viungo vya mtoto huyo wakitafuta Mteja mkoani Kagera.

People are also reading