Home Back

Mfanyabiashara mbaroni tuhuma za kumchoma moto “house girl” kisa wizi

mwanahalisionline.com 2024/10/5
Wilbroad Mutafungwa, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro

MFANYABIASHARA maarufu jijini Mwanza, Christina Shiriri (Manka), anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kumchoma moto mfanyakazi wake wa ndani (House Girl), Grace Joseph, akimtuhumu kwa wizi wa fedha kiasi Cha Sh. 161,000. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Kwa mujibu wa taarifa ya Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza, DCP Wilbroad Mutafungwa, Manka alitekeleza tukio hilo tarehe 4 Juni 2024, baada ya kumwagia Grace  mafuta ya taa mwilini na kumchoma moto.

Taarifa ya Kamanda Mutafungwa imedai kuwa, baada ya Grace kuchomwa moto aliungua maeneo ya mikononi, tumboni na mapajani.

“Manka alidai kuibiwa fedha zake alizokuwa amehifadhi chumbani kwake na alipomuuliza binti yake wa kazi alikiri kuchukua fedha hizo na kuamua kumrejeshea. Baada ya kurejeshewa fedha hizo aliamua kumfanyia ukatili binti huyo kwa kumchoma moto,” imesema taarifa ya Kamanda Mutafungwa.

Kamanda Mutafungwa amesema mtuhumiwa anaendelea kuhojiwa kwa kina na atafikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika.

Kuhusu majeruhi, Kamanda Mutafungwa amesema amepelekwa katika Hospitali ya Wilaya ya Misungwi kwa ajili ya matibabu.

People are also reading