Home Back

Rais Samia apangua Ikulu, wizara, mikia na wilaya

mwanahalisionline.com 2024/7/7

RAIS Samia Suluhu Hassan, amefanya uteuzi na uhamisho wa viongozi mbalimbali, huku sababu ikitajwa ni kuboresha utendaji kazi . Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Mabadiliko hayo ya viongozi yametangazwa Leo Alhamisi na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Moses Kusiluka.

Katika uteuzi huo, Rais Samia amemteua Stanslaus Nyongo, kuwa Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji.

Petro Magoti


Uteuzi huo wa Rais Samia pia umegusa nafasi za makatibu wakuu wa wizara mbalimbali, ambapo amemteua Felister Mdemu, kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi mbalimbali. Katika wizara hiyo, Rais Samia amemteua Amon Mpanju, kuwa Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia masuala ya Jamii na Makundi Maalum.

Rais Samia amemteua aliyekuwa mkurugenzi wa mawasiliano Ikulu, Zuhura Yunus, kuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye ulemavu).

Katika hatua nyingine, Rais Samia amefanya uteuzi na uhamisho wa wakuu wa wilaya, akiwemo Tito Magoti, aliyeteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, akichukua nafasi ya Fatma Nyanhasa aliyehemishiwa Wilaya ya Kondoa.

Dk. Hamis Mkanachi Mkanachi, amehamishwa kutoka kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kondoa kwenda Wilaya ya Urambo, kuchukua nafasi ya Elibariki Bajuta ambaye atapangiwa kazi nyingine.

Hali kadhalika, Rais Samia amewahamisha makatibu tawala wa Mkoa wawili, Reuben Chongolo aliyepelekwa Wilaya ya Mufindi akitijea Songwe. Huku Frank Sichwale aliyekuwa Katibu tawala wa Wilaya ya Mufindi akipelekwa Songwe.

Rais Samia amefanya uhamisho na uteuzi wa wakurugenzi watendaji wa halmashauri Saba.

Miongoni mwa walioteuliwa katika nafasi hiyo ni Mussa Kitunhi, aliyeteuliwa kuwa mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mafia. Kalekwa Kasanga ameteuliwa kuwa mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga.

People are also reading