Home Back

TUCTA wapongeza bajeti ya fedha mwaka 2024/2025

millardayo.com 2024/7/7

Shirikisho la vyama vya wafanyakazi (TUCTA) wameipongeza Serikali Kwa kutenga kiasi cha Shilingi trillion 11.7 Kwa ajili ya kugharamia matumizi ya mishahara ambayo yanajumuisha kupandisha madaraja,ajira mpya,stahiki Mbalimbali za watumishi na nyingeza ya mkupuo kwa watumishi wa umma kwenye bajeti ya mwaka wa fedha 2024/2025.

Akitoa tatarifa Kwa waandishi wa habari Mjini Morogoro Rais wa shirikisho la vyama vya wafanyakazi (TUCTA) Tumaini Nyamhokya amesema serikali imesikia kilio cha wafanyakazi kwenye bajeti ya mwaka ujao 2024/2025 hivyo hatua hiyo inaleta faraja kwa wafanyakazi.

Nyamhokya anasema bajeti hiyo imeenda mbali zaidi na imeainisha kuwa kikokotoo cha malipo ya mkupuo ya pensheni yameongezeka kutoka asilimi 33 ya sasa mpaka 40 ambapo nyongeza hiyo itapunguza malalamiko kwa wafanyakazi.

Aidha ameomba serikali ifanye mchakato wa mabadiliko ya sheria ya hifadhi ya jamii kwa watumishi wa sekta binafsi kutokana na kwamba mabadiliko yaliyopendekezwa hayajagusa wanufaika wa mfuko wa NSSF n bali PSSSF pekee.

Katika hatua nyingine Nyamhokya amewataka wafanyaykazi wa umma na sekta binafsi kuendelea kufanya kazi kwa bidii huku shirikisho hilo likiendelea kuwatete

People are also reading