Home Back

Mwenyekiti Geita auawa na wasiojulikana

ippmedia.com 2024/10/5
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Geita SACP Safia Jongo.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Geita SACP Safia Jongo.

ALIYEKUWA Mwenyekiti wa Mtaa Mwatulole Halmashauri ya Mji wa Geita Noel Ndasa (40), ameuawa na watu wasiojulikana nyumbani kwake majira ya saa 2 usiku wa kuamkia leo Juni 24, 2024.

Watoto wa marehemu pamoja na majirani waliokuwepo eneo la tukio wanadai kuwa walifika wanaume wawili wakiomba kuandikiwa barua ya kusafirisha mifugo, Mwenyekiti huyo alipochukua karatasi na kalamu kutaka kuwaandikia barua ndipo walipoanza kumshambulia kwa mapanga mpaka kifo.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Geita SACP Safia Jongo amethibitisha kutoka kwa tukio hilo huku chanzo cha tukio hilo kikiwa hakijafahamika na hakuna mtuhumiwa anayeshikiliwa mpaka hivi sasa.

People are also reading