Home Back

Bungoma: Askari Auawa na Gari la Polisi Akikagua Lori kwenye Kizuizi cha Barabarani

kiswahili.tuko.co.ke 2024/10/5
  • Fredrick Juma, ambaye anahudumu Kitengo cha Ulinzi wa Miundombinu (CIPU) huko Bungoma, alifariki katika eneo la Cheptais Junction Jumapili, Juni 9
  • Ripoti ya polisi inaonyesha kuwa Juma alikuwa amesimamisha trela kwa ukaguzi wa kawaida alipokanyagwa na gari la polisi
  • Mwili wa marehemu ulihamishwa hadi katika chumba cha kuhifadhi maiti cha Hospitali ya Life Care ukisubiri upasuaji

MAKINIKA: Tusaidie kubadilisha maisha ya wengi, jiunge na programu ya Patreon kutoka TUKO.co.ke.

Bungoma - Polisi wameanzisha uchunguzi baada ya afisa wa trafiki kukanyagwa alipokuwa akitekeleza majukumu yake rasmi katika kaunti ya Bungoma.

Bungoma: Askari Auawa na Gari la Polisi Akikagua Lori kwenye Kizuizi cha Barabarani
Fredrick Juma alifariki dunia papo hapo baada ya kugongwa na gari la polisi. Picha: NPS. Chanzo: UGC

Citizen Digital iliripoti kwamba afisa wa trafiki alifariki papo hapo baada ya kugongwa na gari la polisi eneo la Cheptais Junction Jumapili, Juni 9.

Ripoti ya polisi inasema kuwa Fredrick Juma, ambaye anahudumu katika kitengo cha Ulinzi wa Miundombinu (CIPU) huko Bungoma Magharibi, alisimamisha trela ya Abdullahi Bunyori kwa ukaguzi wa kawaida.

Wakati akimhoji dereva huyo, Juma aligongwa na gari aina ya Toyota Land Cruiser kutoka Kituo cha Polisi cha Sirisia, lililokuwa likitokea upande wa pili.

MAKINIKA: Watumie wahariri wetu taarifa yako unayoiona kuwa bora! Tafadhali wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsApp: 0732482690.

Ripoti hiyo inaeleza kuwa Gideon Magut, akiendesha gari la polisi, alifanikiwa kukwepa kuligonga lori lililokuwa limeegeshwa kando ya barabara.

Afisa huyo wa trafiki alifariki papo hapo baada ya kupata majeraha mabaya kichwani.

"Kutokana na kugongwa, marehemu alitupwa upande wa mbele, akapata majeraha mabaya kichwani na alikufa papo hapo," ripoti ya polisi ilisema kwa sehemu.

Mwili wa marehemu ulihamishwa hadi katika chumba cha kuhifadhi maiti cha Hospitali ya Life Care ukisubiri uchunguzi wa baada ya maiti.

Mengi kufuata...

MAKINIKA: Jinyakulie habari ZINAZOKUFAA ➡️ tafuta na ufurahie!

Chanzo: TUKO.co.ke

People are also reading