Home Back

Namba ya NIDA Kurahisisha Kufungua Akaunti ya Benki ya Equity

globalpublishers.co.tz 2024/10/5

SEKTA ya huduma za fedha ni miongoni mwa sekta zinazokua kwakasi hapa nchini, huku ujumishaji wa watu katika huduma hizo muhimu za kiuchumi ukiongezeka.

Katika kuendelea kuunga mkono jitihada za serikali za kuhakikisha Tanzania inaendana na Mapinduzi ya Kiuchumi kwa kuhakikisha wananchi wanajiunga na kutumia mifumo rasmi ya kibenki, Benki ya Equaity imezindua rasmi mfumo mpya wa kiteknlojia wa kufungua na kupata akaunti rasmi za benki hiyo kwa njia ya simu.

Mfumo huo unatajwa kuwa rahisi na haraka na wenye kuendana na mapinduzi ya Sayansi na Teknolojia katika mageuzi ya mifumo ya kidigitali katika uchumi wa nchi, huku ikilenga kuleta mabadiliko ya njia ya ufunguzi wa akaunti wa hapo awali.

Akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa huduma ya ‘ Hapo Hapo’ Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Malipo Benki ya Equity Aidan Chamshama, amesema huduma hii inamuwezesha mtanzania kufungua akaunti ya Equity popote alipo bila kufika katika tawi, na kujaza fomu, kwa kigezo cha kuwa na namba ya Nida kwa kutumia simu ya mkononi.

Kwa upande wake Meneja benki ya Equity tawi la Mbagala, Salum Halfani amesema akunti hiyo inayofunguliwa kwa njia ya simu ndani ya masaa 24 inatoa huduma zote za kibenki ndani na nje ya nchi.

Mteja wa benki hiyo Teresia Luzige, amesema ufunguzi wa huduma hiyo utarahisiha upotevu wa muda wa kwenda kwenye tawi kufungua akaunti .

People are also reading