Home Back

CCM yampa pole Msigwa, yamuita

ippmedia.com 2024/7/7
news

WAKATI aliyekuwa mgombea uenyekiti wa Kanda ya Nyasa CHADEMA, Mchungaji Peter Msigwa, akitangaza kukata rufani katika chama hicho akidai ushindi aliopata Joseph Mbilinyi ‘sugu’ si halali, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimemuita ajiunge huko kuna demokrasia.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara leo jijini Arusha, ambao ni mwendelezo wa ziara ya Katibu Mkuu CCM, Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi kuzungukia mikoa mitano, Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa, CPA Amos Makala, amempa pole Msigwa na kumwita CCM.

“Kwa hiyo mnaweza kuona wenzetu sasa wana mgogoro mkubwa hakukaliki, mnawasikia wanaleta ubaguzi ni stress (msongo wa mawazo), kuna mgawanyiko mkubwa ndani ya CHADEMA.

“Na sisi Chama Cha Mapinduzi tunaamini kwamba, adui yako muombee njaa, kwa jirani kunawaka moto hakuna haja ya kupeleka maji.

“Sisi tungependa kuwa na vyama vya upinzani vyenye nguvu, lakini katika hili tunaiona fursa ya Chama Cha Mapinduzi kushinda uchaguzi wa Serikali za Mitaa na kushinda Uchaguzi Mkuu unaokuja,” anasema.

Mapema leo katika mkutano alioitisha nyumbani kwake Iringa Mjini, Msigwa amedai kuwa mifumo ya chama chake imetumika kumhujumu ili asishinde.

Amesema kitendo hicho kitaifanya CHADEMA kukosa uhalali wa kuikosoa CCM.

People are also reading