Home Back

Asia: Miaka 20 Bila Figo, Moyo Ulisimama Kwenye Mashine, Aomba Msaada kwa Rais Samia

globalpublishers.co.tz 2024/7/20
Mwanadada Asia Mustafa ambaye kwa takribani miaka 20 sasa, anaishi bila figo.

Hakika kabla hujafa hujaumbika! Kauli hii inamuendea moja kwa moja mwanadada Asia Mustafa @asia.mustafa ambaye kwa takribani miaka 20 sasa, anaishi bila figo kwa sababu figo zake zote zimeharibika na anaishi kwa msaada wa mashine ya kusafisha damu kwenye figo (Dialysis) ambapo ni gharama kubwa sana.

Asia ambaye amewapoteza wazazi wake wote wawili ambao ndiyo walikuwa msaada mkubwa katika maisha yake, hivyo hana tegemeo lingine, na kwa sababu ya kwenda kwenye mashine kwa muda mrefu, mifupa yake imepata tatizo na kutobokatoboka na kusababisha kushindwa kutembea tena.

“Sina wa kumtegemea hata hela ya dialysis naombaomba kwa marafiki zangu na sasa hivi nafanya kusafisha damu kwenye figo mara moja tu na inatakiwa mara tatu, naomba msaada wa bima utaweza kunisaidia sana, nateseka mno na ninapoishi ni mbali na hospitali hivyo inanilazimu usafiri tu kutumia 60,000, bado kulipia gharama za kusafisha damu,” alisema Asia.

Kama umeguswa msaidie Asia chochote kupitia namba yake 0656684431 (Asia Salih).

People are also reading