Home Back

Airtel Money Kurahisisha Malipo ya Ada za shule kidijitali

mtaakwamtaa.co.tz 2024/10/5

 

Mkurugenzi wa Airtel Money Tanzania, Andrew Rugamba katikati, kutoka kulia wapili ni Mkurugenzi wa Shule ya Fountain Gate, Japhet Makau na wafanyakazi wa Airtel Money wakifurahia uzinduzi wa ‘Airtel Money School Pay’ jijini Dar es Salaam leo Juni 27, 2024.

Mkurugenzi wa Airtel Money Tanzania, Andrew Rugamba katikati, kutoka kulia wapili ni Mkurugenzi wa Shule ya Fountain Gate, Japhet Makau na wafanyakazi wa Airtel Money wawakifurahia uzinduzi wa ‘Airtel Money School Pay’ jijini Dar es Salaam leo Juni 27, 2024.

Picha ya Pamoja mara baada ya uzinduzi wa  ‘Airtel Money School Pay’ jijini Dar es Salaam leo Juni 27, 2024.

KATIKA kuhakikisha wanaunga mkono juhudi za serikali kufikia uchumi wa kidijitali kwa kupunguza matumizi ya fedha taslimu (cashless economy), Airtel Money Tanzania leo imezindua ‘Airtel Money School Pay’ huduma ya malipo kidijitali yenye lengo la kurahisha mchakato wa ulipaji wa Ada katika shule mbalimbali.

Akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam leo Juni 27, 2024 Mkurugenzi wa Airtel Money Tanzania, Andrew Rugamba wakati wa kutambulisha ‘Airtel Money School Pay’ amesema kuwa huduma hiyo itasaidia kuongeza usalama na njia madhubuti kwa wazazi na walezi ili kuweza kufanya malipo ya ada shuleni akiwa popote nchini.

Rugamba amesema kuwa Huduma hiyo imeundwa mahususi kwa shule binafsi ili kurahisisha malipo na kutunza kumbukumbu wakati wowote.

“Wazazi sasa wanaweza kulipa ada za shule kwa urahisi kupitia simu zao za mkononi, wakati wowote na mahali popote kutokana na kuunganishwa kwa teknolojia ya malipo ya simu ya Airtel Money School Pay. Shule binafsi kote nchini zitaweza kukusanya ada moja kwa moja kwenye akaunti zao za benki, na hivyo kuwezesha njia bora katika usimamizi wao wa fedha.” Ameeleza Rugamba

Pia amesisitiza umuhimu wa huduma ya malipo ya Airtel Money School School, huku akieleza kuwa ni hatua kubwa ya kuimarisha usalama na usimamizi wa malipo shuleni, hasa kwa wazazi na shule za Tanzania.

“Tumejitolea kutoa suluhisho la kibunifu litakalorahisisha malipo baina ya wazazi, walezi na shule katika swala la ulipaji karo. Airtel Money School Pay ni mfano dhahiri wa jinsi Airtel Money inavyowapa kipaumbele wateja wake kwa kurahisisha na kuboresha maisha yao. Mfumo huu ni wa kipekee na una huduma za ziada kama Mifumo ya usimamizi wa ada, mfumo wa usimamizi wa wanafunzi, na mfumo wa usimamizi na kutunza kumbukumbu za uhasibu, Mifumo yote hiyo inatolewa bila malipo kwa shule zinazotumia mfumo huu wa Airtel Money School Pay. Wazazi wanaweza kuepuka foleni ndefu na kulipa ada kwa urahisi kupitia simu zao. Huu mfumo unahakikisha miamala inafanyika kwa salama na kupunguza hatari zinazohusiana na utunzaji wa pesa.” Ameleza.

Baadhi ya shule kibinafsi nchini zishaanza kutumia mfumo huu, ambao unawawezesha wazazi kufanya malipo ya karo ya shule. Shule hizo ni pamoja na Shule za Fountain Gate, Ubungo Islamic High School, na Shule ya Sheikhat Hissa.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Shule ya Fountain Gate, Japhet Makau, ametoa shukrani zake kwa Airtel Money kwa kuanzisha mfumo ambao unahakikisha usalama wa miamala ya malipo ya ada kutoka kwa wazazi na walezi.

"Mfumo wa Airtel Money School Pay umeboresha kwa kiasi kikubwa utaratibu wetu wa kukusanya ada na pia umeimaisha usimamizi wetu wa fedha kwa kutoa muda wa kupokea uthibitisho wa papo kwa hapo ada zilizolipwa na vipengele vya ziada vimesaidia usimamizi wote bila matatizo," Makau amesema.

Ameongeza “Malipo ya ada kupitia Airtel Money School Pay inatusaidia kuacha kutumia karatasi kwa sababu ni mfumo wa kisasa wa kufanya malipo na unaojiendesha kwa mtandao; hii itachangia kutunza zaidi mazingira yetu. Taarifa zetu zitakuwa kwa mpangilio mzuri na kuondoa kero ya kutunza nyaraka kwa ajili ya marejeleo kwa kuwa mfumo huu upo kidijitali, wazazi na wanafunzi hawatohitaji kubeba au kuhifadhi kumbukumbu za malipo na risiti ili kufuatilia na kuhakikisha malipo yao yamefika shule.”

Wazazi na walezi wanaweza kupata huduma ya Airtel Money School Pay kwa kupiga *150*60#, chagua chaguo 5 (Fanya Malipo), chagua Ada ya Shule, kisha uchague chaguo la 3 (School Pay) ili kuendelea na malipo.

People are also reading