Home Back

Rais Samia atunukiwa Shahada ya heshima ya Udaktari wa Falsafa

ippmedia.com 2024/7/7
Rais Samia Suluhu Hassan akitunukiwa Udaktari wa Falsafa wa Heshima (Honoris Causa) kwenye Sekta ya Anga na Rais wa Chuo Kikuu cha Sayansi ya Anga (Korean Aerospace University) Hee Young Hurr, Jijini Seoul, Jamhuri ya Korea leo Juni 03,2024.

Rais Samia Suluhu Hassan akitunukiwa Udaktari wa Falsafa wa Heshima (Honoris Causa) kwenye Sekta ya Anga na Rais wa Chuo Kikuu cha Sayansi ya Anga (Korean Aerospace University) Hee Young Hurr, Jijini Seoul, Jamhuri ya Korea leo Juni 03,2024.

RAIS Samia Suluhu Hassan, ametunukiwa Shahada ya Heshima ya Udaktari wa Falsafa (Doctorate Honoris Causal) na Chuo Kikuu cha Anga Korea (KAU) kwa kutambua mchango wake katika mabadiliko ya sera na uongozi wa kimantiki.

Shahada hiyo imetolewa leo katika hafla maalum iliyoandaliwa na chuo hicho na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Korea na Tanzania.

Hii ni shahada ya heshima ya tano wa Rais Samia baada ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Chuo Kikuu Zanzibar (SUZA), Chuo Kikuu cha Jawaharial Nehru cha India na Chuo Kikuu cha Ankara, Uturuki, wote wakitambua mchango wake kwenye nyanja mbalimbali.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akitunukiwa Udaktari wa Falsafa wa Heshima (Honoris Causa) kwenye Sekta ya Anga na Rais wa Chuo Kikuu cha Sayansi ya Anga (Korean Aerospace University) Hee Young Hurr wa kwanza kulia, Jijini Seoul, Jamhuri ya Korea.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akitunukiwa Udaktari wa Falsafa wa Heshima (Honoris Causa) kwenye Sekta ya Anga na Rais wa Chuo Kikuu cha Sayansi ya Anga (Korean Aerospace University) Hee Young Hurr, Jijini Seoul, Jamhuri ya Korea tarehe 03/06/2024.
People are also reading