Home Back

Tetesi za Soka Ulaya Ijumaa 05.07.2024

bbc.com 2024/10/5

Chanzo cha picha, Reuters

Ederson
Maelezo ya picha, Kipa wa City Ederson

Manchester City wanajiandaa kupokea ombi la Saudi Arabia kumnunua mlinda mlango Ederson na wanataka zaidi ya pauni milioni 30 kumuuza mchezaji huyo wa kimataifa w a Brazil, ambaye anahusishwa na klabu ya Al-Nassr. (Sportsport)

Marseille wana uhakika wa kuwashinda Lazio kumsajili mshambuliaji wa Manchester United Mason Greenwood baada ya klabu hiyo ya Serie A kutoa pauni milioni 17 kwa mchezaji huyo wa miaka 22 (Mail)

Flamengo ilianza mawasiliano na West Ham kuhusu usajili wa mchezaji wa kimataifa wa Brazil mwenye umri wa miaka 26 Lucas Paqueta na klabu hizo mbili ziko katika hatua za awali za mazungumzo. (Globo)

Chanzo cha picha, Getty Images

Mason Greenwood
Maelezo ya picha, Marseille wana uhakika wa kuwashinda Lazio kumsajili mshambuliaji wa Manchester United Mason Greenwood

Barcelona wanaongoza mbio za kumsajili winga wa Athletic Bilbao na Uhispania Nico Williams, huku Arsenal na Chelsea wakikabiliwa na hatari ya kumkosa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21. (Football Insider)

Beki wa Chelsea Marc Cucurella, 25, anasema anajaribu kumshawishi mchezaji mwenzake wa Uhispania Williams ajiunge na The Blues, wawili hao wakiwa kwenye kikosi cha nchi yao kwenye Euro 2024. (Sport -kwa Kihispania)

Beki wa Lille Leny Yoro anataka kuhamia Real Madrid na Mfaransa huyo mwenye umri wa miaka 18 anasubiri vilabu kuafikiana, wakati Liverpool na Paris St-Germain ziko tayari kunyakua iwapo dili hilo litasambaratika. (Fabrizio Romano)

Beki wa kulia wa Aston Villa Matty Cash huenda asijiunge na AC Milan licha ya ripoti zinazomhusisha mchrzaji huyo wa kimataifa wa Poland mwenye umri wa miaka 26 na klabu hiyo ya Serie A. (Birmingham Live)

Barcelona wana hamu ya kumsajili Joao Cancelo wa Manchester City baada ya beki huyo wa Ureno mwenye umri wa miaka 30 kucheza kwa mkopo katika klabu hiyo ya Uhispania msimu uliopita. (SportsMole)

Juventus wanataka kuimarisha safu yao ya kati kwa kumsajili mchezaji wa kimataifa wa Uholanzi mwenye umri wa miaka 26 Teun Koopmeiners. (La Gazzetta dello Sport - kwa Kiitaliano)

Manchester United wanakaribia kumsajili kinda mwenye umri wa miaka 16 kutoka Slovakia Samuel Lusale kutoka Crystal Palace. (Kioo)

xx

Chanzo cha picha, Getty Images

Uhamisho wa Newcastle United wa mshambuliaji wa Everton Dominic Calvert-Lewin, 27, umegonga mwamba baada ya Magpies kushindwa kumuuza mshambuliaji wao Mwingereza Callum Wilson. (Telegraph - usajili unahitajika)

Ajax, Nice, Rennes na Olympiakos ni miongoni mwa klabu kadhaa zinazovutiwa na mlinzi wa Ureno Cedric Soares, 32, ambaye ni mchezaji huru baada ya kumalizika kwa mkataba wake na Arsenal. (Standard)

Brighton walichukua fursa ya kuchelewesha kwa Liverpool katika kukamilisha dili la kiungo wa Feyenoord Mats Wieffer baada ya mkufunzi wa Reds Arne Slot kuonyesha ishara ya kuungana na Mholanzi huyo mwenye umri wa miaka 24 kuwa pamoja katika klabu hiyo ya Uholanzi. (De Telegraaf)

xx

Chanzo cha picha, Getty Images

Manchester United wanataka kumuuza kiungo wa kati wa Uholanzi Donny van de Beek msimu huu badala ya kumpoteza kwa uhamisho wa bure wakati mkataba wa mchezaji huyo wa miaka 27 utakapokamilika msimu ujao wa joto. (Manchester Evening News)

Mshambuliaji wa Chelsea Romelu Lukaku, 31, anataka kuungana na mkufunzi wa Napoli Antonio Conte, ambaye alimfundisha mchezaji huyo kwa kimataifa wa Ubelgiji katika klabu ya Inter Milan. (Corriere dello Sport - kwa Kiitaliano)

Napoli wameiambia Chelsea kuwa wako tayari kupunguza bei yao ya £110.8m kwa mshambuliaji wa Nigeria Victor Osimhen, 25. (Metro)

Beki wa Ujerumani Waldemar Anton, 27, amefuzu vipimo vya afya katika klabu ya Borussia Dortmund na atajiunga nao kutoka klabu ya Stuttgart ya Ujerumani baada ya Euro 2024. (Sky Sports Germany)

People are also reading