Home Back

Balozi Yakubu awasilisha Hati za Utambulisho kwa Rais wa Comoro

mwanahalisionline.com 4 days ago

Balozi wa Tanzania nchini Comoro, Saidi Yakubu, leo Jumanne amewasilisha hati za utambulisho kwa Rais wa Nchi hiyo, Azali Assoumani ambapo wamepata pia fursa ya kufanya mazungumzo kuhusu uhusiano wa nchi hizo mbili. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Balozi Yakubu ambaye aliwasilisha hati hizo za utambulisho kwa lugha ya Kikomoro jambo lililomfurahisha Rais Azali alitumia pia fursa ya utambulisho kuwasilisha pia salamu za Rais Samia Suluhu Hassan za nia yake ya kuona ushirikiano wa Tanzania na Comoro unaongezeka.

Kwa upande wake Rais Azali alimueleza Balozi Yakubu kuwa Comoro inathamini uhusiano wa kindugu na kihistoria baina yake na Comoro na kuwa daima watauenzi uhusiano huo na kumtaka atumie uwepo wake kuboresha ushirikiano wa kibiashara,kiuchumi,kijamii na kisiasa pia.

Awali kabla ya uwasilishaji wa hati za utambulisho Balozi Yakubu alikagua gwaride la heshima lililoandaliwa.

People are also reading