Home Back

Mrembo Awagiwa Tindikali Arusha Alazwa katika Hospitali ya Mount Meru

globalpublishers.co.tz 3 days ago
Mwanadada Jackline Lauo.

Mwanadada Jackline Lauo anayefanya kazi ya kuuza duka la nguo katika Mtaa wa Nazi, jirani na Stendi Kuu ya Arusha amelazwa katika Hospitali ya Mount Meru baada ya kumwagiwa kimiminika kinachodhaniwa kuwa ni tindikali.

Akizungumza kwa maumivu makali, Jackline ameeleza kuwa tukio hilo lilitokea Juni 6, 2024 ambapo akiwa anatoka kazini kwake, watu wawili waliokuwa wamepakizana kwenye bodaboda, walimfanyia ukatili huo na kutokomea kusikojulikana.

People are also reading