Home Back

Rais Samia Ampokea Rais wa Msumbiji, Filipe Jacinto Nyusi Ikulu jijini Dar (Picha +Video)

globalpublishers.co.tz 2024/10/5
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Samia Suluhu Hassan akiwa na mgeni wake Rais wa Msumbiji Filipe Jacinto Nyusi mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Samia Suluhu Hassan, amempokea Rais wa Jamhuri ya Msumbiji, Filipe Jacinto Nyusi, katika hafla ya mapokezi rasmi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam leo, tarehe 02 Juni 2024.

Wakati wa mapokezi hayo,  Rais Nyusi alikagua gwaride rasmi lililoandaliwa kwa heshima yake pamoja na kupigiwa mizinga 21.

Kadhalika, MRais Nyusi alipata fursa ya kusaini kitabu cha wageni pamoja na kushiriki mazungumzo ya faragha na mwenyeji wake, Rais Samia, yaliyofuatiwa na mazungumzo rasmi yaliyowashirikisha viongozi mbalimbali kutoka Tanzania na Msumbiji.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na viongozi mbalimbali mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 02 Julai, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa amesimama pamoja na mgeni wake Rais wa Msumbiji Mhe. Filipe Jacinto Nyusi wakati Wimbo wa Taifa wa Tanzania ukiimbwa kwenye mapokezi Rasmi yaliofanyika katika viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 02 Julai, 2024.
Rais wa Msumbiji Mhe. Filipe Jacinto Nyusi akikagua Gwaride la Heshima lililoandaliwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 02 Julai, 2024.
Rais wa Msumbiji Mhe. Filipe Jacinto Nyusi akisaini Kitabu cha Wageni mara baada ya kuwasili Ikulu Jijini Dar es Salaam 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na mgeni wake Rais wa Msumbiji Mhe. Filipe Jacinto Nyusi Ikulu Jijini Dar es Salaam 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Rais wa Msumbiji Mhe. Filipe Jacinto Nyusi Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 02 Julai, 2024.
People are also reading