Home Back

DP Gachagua avunja kimya ajibu matamshi ya Ichungw'a

radiojambo.co.ke 2024/10/6
Wale wanaopinga siasa zake wamemshutumu DP kwa kuendeleza ukabila kwa gharama ya kuunganisha nchi.
Muhtasari
  • Akizungumza alipohutubia Kongamano la Kimataifa la Chama cha Madawa ya Kenya mjini Mombasa siku ya Jumatano, Gachagua alisema kuwa atarejea kijijini kila mara baada ya kazi.

Naibu Rais Rigathi Gachagua amewasuta wakosoaji wake na kuwaambia hatakwepa kujivunia kabila lake.

DP, ambaye amekuwa chini ya shinikizo kubwa kutokana na matamshi kwamba anadaiwa kuendeleza ukabila, alisema kila Mkenya anafaa kujivunia lugha yake ya asili.

"Kila mtu anapaswa kujivunia asili yako na utambulisho wako, hakuna mtu anayefaa kukufanya uhisi aibu kuhusu asili yako na utambulisho wako," Gachagua alisema.

Akizungumza alipohutubia Kongamano la Kimataifa la Chama cha Madawa ya Kenya mjini Mombasa siku ya Jumatano, Gachagua alisema kuwa atarejea kijijini kila mara baada ya kazi.

“Sitaki kusema mengi, nataka niende Nairobi kwa muda mfupi kisha niende kijijini,” alisema.

"Sijui kwa nini mtu yeyote atakuwa na tatizo na tunakotoka.''

Kauli hiyo inaonekana kuwa jibu la moja kwa moja kwa wakosoaji wake ambao wametilia shaka aina yake ya siasa ambayo wanadai kuwa ni ya Mlima Kenya licha ya kuwa ana afisi ya kitaifa.

Wale wanaopinga siasa zake wamemshutumu DP kwa kuendeleza ukabila kwa gharama ya kuunganisha nchi.

Siku ya Jumatano, DP alijibu akisema Wakenya hawafai kuonea aibu kabila lao kwa sababu kila mtu ni wa eneo au kabila fulani.

"Kila mtu ako na kwao, hii Mombasa na Nairobi ni kiwanja ya kutafuta riziki, lakini mwisho kabisa unajua utarudi,'alisema.

DP alionya wapinzani na wakosoaji wake kutowaadhibu wengine kwa sababu tu wanazungumza kwa lugha yao ya kwanza au wanazungumza na watu wa kabila zao.

People are also reading